Tshishimbi aahidi ubingwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Nov 2019
Tshishimbi aahidi ubingwa Yanga

Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi amewaomba radhi mashabiki baada ya timu yao kuondoshwa kwenye michuano ya kombe la Shirikisho kwa kufungwa jumla ya mabao 5-1 na Pyramids Fc

Tshishimbi amesema matokeo hayo hayawakatishi tamaa, bali yatakuwa chachu kwao kupambana ili waweze kufanya vizuri wapate nafasi ya kushiriki tena michuano hiyo msimu ujao

"Tunawaambia mashabiki wetu kuwa hatuwezi kukata tamaa, najua hii sio mara ya kwanza na ya mwisho kwa Yanga kufungwa. Tutahakikisha tunajituma ili tuweze kutwaa ubingwa mwakani tushiriki tena"

"Tunawaomba mashabiki waendelee kutuunga mkono, ni matokeo ya mpira wa miguu wakati mwingine hayawi ya kufurahisha. Nafahamu mtu ukishapenda timu utaishabikia hiyo hiyo huwezi kuhama"

"Hivyo naomba wazidi kutuunga mkono, sisi tutaendelea kupambana, tunaanza matayarisho kwa ajili ya ligi. Tutakwenda Mtwara tukiwa na malengo ya kupata ushindi, Hatuwezi kukubali kufungwa mara tatu mfululizo, " amesema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’