Walinzi Lamine Moro na Ally Ally wameongeza idadi ya majeruhi baada ya kuumia kwenye mchezo wa jana dhidi ya Pyramids Fc
Lamine alicheza mchezo wa jana akiwa bado hajapona vizuri majeraha ya nyama za paja
Ally Ally aliumia kwenye dakika ya 70, alianguka vibaya wakati akiwania mpira wa juu na mchezaji wa Pyramids Fc
Bado Mohammed Issa 'Banka' na Paulo Godfrey 'Boxer' wameendelea kuwa nje kwa muda mrefu
Issa Bigirimana na Raphael Daudi wamekuwa wakipona na kurudi katika majeraha kila baada ya muda
Hivi karibuni Maybin Kalengo naye alipata majeraha ambayo yatamuweka nje kwa miezi mitatu
Wingi wa majeruhi imekuwa changamoto kwa klabu ya Yanga tangu msimu uliopita
Msimu huu kuna wakati Yanga ilikuwa na majeruhi 12!
Uongozi wa Yanga ulifanya mabadiliko benchi lake la matibabu ya wachezaji ambapo Dk Sheki Mgazija alichukua nafasi ya Dk Edward Bavu
Changamoto kubwa inayoonekana ni muda ambao wachezaji wanachukua kupona baada ya kuumia