Msafara wa kikosi cha Yanga unaondoka nchini leo kuelekea Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Novemba 03 katika uwanja wa June 30
Yanga inatarajiwa kuondoka na msafara wa wachezaji 20. Aidha tayari baadhi ya viongozi walishatangulia nchini humo kuweka sawa mapokezi ya kikosi hicho
Kocha Mwinyi Zahera amesema watakuwa na siku mbili za kufanya maandalizi Misri kabla ya kuwakabili Pyramids ambao wana faida ya ushindi wa mabao 2-1 waliopata nchini
Yanga inahitaji kushinda kuanzia mabao mawili au zaidi ili iweze kutinga makundi
ADVERTISE HERE