Pyramids wanafungika hukohuko kwao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Oct 2019
Pyramids wanafungika hukohuko kwao

Licha ya Yanga kutopewa nafasi kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa Jumapli, Novemba 03 huko Misri, Yanga inaweza kufanya maajabu

Baada ya kufungwa mabao 2-1 nyumbani, hawapewi nafasi ya kupindua matokeo Misri

Lakini kiuhalisia jambo lolote linaweza kutokea nchini Misri kutokana na mazingira ya mchezo huo

Pamoja na ubora wao, Pyramids Fc wanaweza kufungwa hukohuko kwao

Katika michezo miwili waliyocheza kwenye uwanja wa nyumbani kwenye michuano ya kombe la Shirikisho msimu huu, wameshinda mmoja na kutoka sare mmoja

Waliifunga Etoile Du Congo mabao 4-1 katika mchezo wa hatua ya awali na baadae kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya CR Belouizdad

Pyramids inaonekana kuwa imara sana inapocheza ugenini kuliko nyumbani kwani imeshinda mechi zote tatu za ugenini. Wakati kwa upande wa Yanga ilitinga raundi ya kwanza kwa kushinda ugenini na kupoteza kwa 'bahati mbaya' nchini Zambia kwa bao la kujifunga la Makame

Pyramids wameruhusu bao katika kila mechi waliyocheza nyumbani kwenye michuano hii

Yanga itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na hesabu ya kufunga angalau mabao mawili

Ushindi wa mabao 2-0 ugenini utaipeleka Yanga hatua ya makundi

Matokeo ya 2-1 yataupeleka mchezo huo kwanye matuta wakati kama Yanga watapata ushindi wowote wa kuanzia mabao matatu, watafuzu

Jambo jema ni kuwa Yanga sio ngeni kucheza Misri

Katika kipindi cha miaka mitano imeshacheza na Al Ahly na Zamelek kwenye uwanja huo wa June 30

Mchezo wa Jumapili wachezaji wa Yanga watakuwa huru kwani hawana cha kupoteza baada ya kufungwa mchezo wa nyumbani

Kocha Mwinyi Zahera amesema mapema kuwa mbinu za mchezo huo hazitakuwa sawa na walivyocheza mechi ya kwanza

"Tunajua tunapaswa kushinda, haitakuwa rahisi lakini tunaowachezaji ambao wanaweza kutupa matokeo, lolote linaweza kutokea," alisema Zahera

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’