Zahera azungumzia tukio la kutupiwa makopo Mwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Oct 2019
Zahera azungumzia tukio la kutupiwa makopo Mwanza

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema hana tatizo na mashabiki waliomtukana na kumrushia makopo jijini Mwanza baada ya Yanga kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Pyramids Fc

Zahera ambaye amerejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo wa marudiano ambao utapigwa Novemba 03, amesema anafahamu siku zote mashabiki wa soka wanachohitaji ni ushindi tu

"Mimi sina tatizo na tukio lile, nafahamu mashabiki walikuwa na hasira baada ya timu yao kufungwa. Msimu uliopita hata kocha wa Simba mashabiki hawahawa si walimtupia makopo lakini baadae si alikuja kutwaa ubingwa?," aliongeza Zahera

Hata hivyo Zahera amesisitiza pamoja na timu kupoteza mchezo, wachezaji wake wanastahili pongezi kutokana na kazi kubwa waliyofanya

"Kuna nyakati hatukucheza vizuri na muda mwingine tulicheza vizuri. Lazima tukubali, tulicheza na timu bora zaidi yetu, vijana wangu walifanya kazi kubwa na niliwapongeza sana baada ya mchezo"

"Tulifanya maandalizi ya kutosha kuwakabili, kupoteza mchezo ni matokeo ya bahari mbaya ambayo yalisababishwa na makosa ya kupoteza umakini"

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’