Tumefungwa kwa bahati mbaya - Zahera

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Oct 2019
Tumefungwa kwa bahati mbaya - Zahera

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amewapongeza wachezaji wake kwa kuipigania timu kwenye mchezo wa jana kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc licha ya kipigo cha mabao 2-1

Zahera amesema Yanga ilipoteza mchezo huo kwa bahati mbaya, lakini pia walikutana na timu ambayo ilikuwa bora zaidi yao

Zahera amesisitiza kuwa uongozi wa timu hiyo ulifanya uamuzi sahihi wa kubadili uwanja kutoka Taifa kwenda CCM Kirumba kwani uwanja haukuwa sababu ya wao kufungwa

"Mabadiliko ya uwanja haikuwa tatizo, " Zahera amewaambia waandishi wa habari muda mfupi baada ya kurejea jijini Dar es salaam

"Ukiangalia tumekosa bahati katika michezo hii. Angalia mchezo dhidi ya Zesco kule Zambia, goli la pili tulijifunga kwa bahati mbaya"

"Jana inatokea tena bahati mbaya, Ngasa aliwaza kama ukiuacha ule mpira utatoka, tumefungwa sababu ya bahati mbaya"

"Sasa kama wewe unafungwa kwa bahati mbaya, unafungwa na timu ambayo ni bora zaidi yako, huwezi kulalamika zaidi ya kukubali matokeo"

"Wachezaji wanastahili pongezi kwani walijitolea nguvu yao yote kuhakikisha timu inafanya vizuri lakini tumekosa bahati"

Yanga imerejea jijini Dar es salaam kuendelea na maandalizi ya mchezo wa marudiano ambao utapigwa Jumamosi, Novemba 03 nchini Misri

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
2m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
23h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’