Yanga imeshindwa kuutumia vyema uwanja wake wa nyumbani baada ya kukubalki kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Pyramids Fc ya Misri
Pyramids walitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye kipindi cha kwanza ambacho walikitawala kwa muda mwingi
Kipindi cha pili Yanga ilirejea ikiwa imara zaidi ikisaka bao la kusawazisha hata hivyo makosa yaliyofanywa na winga Mrisho Ngasa aliyeuacha mpira aliodhania umetoka, yaliigharimu Yanga kwa kufungwa bao pili na hivyo kujiongezea mzigo mara dufu
Pamoja na kufungwa mabao mawili, vijana wa Yanga walionekana kuwa watulivu wakipeleka mashambulizi kusaka bao

Aidha kuingia kwa Juma Balinya na Patrick Sibomana kuliiongezea Yanga kwenye ushambuliaji
Papy Tshishimbi aliifungia Yanga bao pekee dakika ya 89 akimalizia mpira uliotengwa na Balinya
Yanga ilimaliza mchezo ikiwa na wachezaji 10 baada ya beki Kelvin Yondani kutolewa nje kwa kadi nyekundu wakati mchezo unaelekea ukingoni
Ili kuweza kusonga mbele Yanga inahitaji kufunga angalau mabao mawili ugenini