Majeruhi yatajwa sababu ya kikosi pungufu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Oct 2019
Majeruhi yatajwa sababu ya kikosi pungufu Yanga

Ukiangalia orodha ya wachezaji wa kikosi cha Yanga ambacho kitaivaa Pyramids Fc muda mchache ujao, wachezaji wako 17, wachezaji 11 wakianza na sita wakiwa benchi badala ya saba

Hata hivyo kati ya hao sita walio nje, magolikipa ni wawili Metacha Mnata na Ramadhani Kabwili

Ni dhahiri changamoto hiyo imesababishwa na wimbi la majeruhi

Wengi wameshangazwa kukosekana kikosini kwa mshambuliaji Juma Balinya ambaye hayuko hata kwenye wachezaji wa akiba

Ingawa uongozi wa Yanga haujatoa taarifa rasmi, Mshambuliaji huyo huenda amepata majeraha kuelekea mchezo huo kwani hakukuwa na sababu ya kukosekana miongoni mwa wachezaji wa akiba kwani hata waliopo wako pungufu

Beki Lamine Moro anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano wakati Mustafa Suleyman na David Molinga wao hawana vibali

Ilitangazwa mapema kuwa wachezaji Paulo Godfrey, Mohammed Issa, Issa Bigirimana, Maybin Kalengo na Raphael Daudi ni majeruhi

Pia ikumbuke wachezaji wenye sifa ya kushiriki michuano hii ni wale waliosajiliwa CAF, wengine wanaweza kuwa wamesajiliwa kwa ajili ya ligi lakini hawana sifa ya kucheza michezo hii mfano Gustava Saimon na Cleofas Sospeter

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’