Mapinduzi Balama ni mmoja wa nyota wapya waliosajiliwa na Yanga dirisha la usajili msimu huu, amekuwa katika kiwango bora
Pamoja na usajili wa nyota wengi wa kigeni, Balama amejihakikishia namba kwenye kikosi cha kwanza na ameitendea haki heshima hiyo anayopewa na kocha Mwinyi Zahera
Leo Balama anaangaliwa kama mchezaji muhimu sana kuelekea mchezo dhidi ya Pyramids Fc
Kasi yake inaweza kuwa tatizo kwa Waarabu hao ambao waliwasili juzi Ijumaa

Lakini pia Balama ameonyesha kuwa uwiano mzuri wa kushambulia na kuzuia, haishangazi kuona kwa nyakati tofauti Zahera alimtumia kama mlinzi wa kulia
Mchezo wa leo unahitaji wachezaji wa aina yake ambao wanaweza kuongoza mashambulizi na kurudi kwa haraka kujilinda pale inapobidi
Kwani pamoja na Yanga kuhitaji ushindi, inahitaji kuwa na nidhamu katika kujilinda ili kuhakikisha Pyramids hawapati bao la ugenini