Shamrashamra zashamiri Mwanza

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Oct 2019
Shamrashamra zashamiri Mwanza

Ukiwa jijini Mwanza wakati huu unaweza ukadhani kuna sherehe ya Kitaifa lakini ukweli ni kwamba ni shamrashamra za Wananchi wakiwa njiani kuelekea CCM Kirumba ambako baadae timu yao itachuana na Pyramids Fc kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho

Ari ya mashabiki iko juu, wengi wamehamasika na kufurahia uamuzi wa Yanga kuupeleka mchezo huo Mwanza

Hakika hii ni siku muhimu kwa Wanayanga wa Mwanza na Tanzania kwa ujumla, siku hii itapendeza zaidi kama ushindi utapatikana Kirumba baadae

Pamoja na uwepo wa mashabiki wachache wa Simba ambao wamepanga kwenda Kirumba kuishangilia Pyramids Fc, 'nyomi' la Wanayanga litawapoteza kabisa

Mjumbe wa Kamati ya uhamasishaji Jimmy Kindoki amewataka mashabiki wa Yanga kuingia mapema uwanjani kuchukua nafasi majukwaani ili kuwakwamisha wapinzani wao waliopanga kwenda kuwapa sapoti Pyramids Fc

Tayari mageti ya uwanja wa CCM Kirumba yamefunguliwa na mashabiki wameanza kuingia

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
23h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’