Mashabiki washauriwa wachangamkie tiketi mapema

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Oct 2019
Mashabiki washauriwa wachangamkie tiketi mapema

Mashabiki wa klabu ya Yanga jijini Mwanza wametakiwa kuchangamkia kununua tiketi mapema ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza Jumapili ambayo ni siku ya mchezo dhidi ya Pyramids Fc

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema tiketi zinaanzwa kuuzwa leo kupitia vituo vilivyoainishwa na klabu hiyo jana

Viingilio vya mchezo huo ambao utapigwa saa 10 jioni ni Royal Tsh 50,000/-, VIP Tsh 20,000/- na Mzunguuko Tsh 7,000/-

"Mashabiki wachangamke mapema kununua tiketi ili siku ya Jumapili wawe na zoezi moja tu, kwenda uwanjani kuishangilia timu yao," amesema

"Hii itawaepusha na changamoto zinazoweza kujitokeza siku ya mchezo. Tutafunga zoezi la kuuza tiketi Jumapili mchana lakini inaweza kuwa mapema zaidi kama tiketi zitamalizika"

Vituo vinavyouza tiketi

1. Nyamagana

2. Kituo cha mabasi Nyegezi

3. Kituo cha mabasi Buzuruga

4. Kituo cha mabasi Igoma

5. Shule ya Msingi Buhongwa

6. Uwanja wa CCM Kirumba

7. Lenana Hotel Pasiasi

8. Posta Pamba Road

9. Kituo cha mabasi Mkolani

10. Kituo cha mafuta Buswelu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’