Kamusoko haondoki Yanga

Admin By Admin
•
27 Jun 2017
Kamusoko haondoki Yanga
Kiungo wa Kimataifa wa Zimbabwe anayekipiga na mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga, Thabani Kamusoko amesema atasaini mkataba mpya kuendelea kuitumikia Yanga.

Katika mahojiano na mtandao wa GOAL, Kamusoko amekiri kupokea ofa mbalimbali kutoka Tanzania na nje ya Tanzania lakini atasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Yanga.

“Mashabiki wa Yanga waondoe hofu juu yangu nitabaki hapa kwa sababu kitu nilichohitaji ambacho ni ubingwa wa Afrika au hata kucheza fainali bado sijapata na naamini msimu ujao tunaweza kufanya vizuri na kutimiza hilo,” amesema Kamusoko.

Kiungo huyo amesema anaimani kubwa na wachezaji wapya watakaosajiliwa na timu hiyo kuwa wataongeza nguvu na kufanya vizuri pale waliposhindwa hasa kwenye michuano ya kimataifa.

Kamusoko amesema anatambua kuwa msimu ujao utakuwa mgumu kwao kutokana na timu nyingi kujiandaa lakini watafanya maandalizi mazuri chini ya kocha wao George Lwandamina na kufanya vizuri ikiwepo kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Yanga kwa sasa ipo katika wakati mgumu kuhakikisha inawabakiza nyota wake waliomaliza mikataba, baada ya wapinzani wao Simba kuonekana kuwanyemelea na tayari imeshafanikiwa kumchukua kiungo wake wa kimataifa Haruna Niyonzima raia wa Rwanda.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
14h ago
READ MORE →
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
14h ago
READ MORE →
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
18h ago
READ MORE →
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
18h ago
READ MORE →
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE →
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
23h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE →