Hatusajili hovyo hovyo - Mkwassa

Admin By Admin
•
13 Jun 2017
Hatusajili hovyo hovyo - Mkwassa
Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwassa amesema klabu hiyo imeachana na tabia ya kusajili wachezaji bila ya kuangalia mahitaji na mapendekezo ya kocha.

Mkwassa ametoa kauli hiyo wkaati ambapo kuwekuwa na maneno maneno kuwa 'ukata' ulioikumba klabu hiyo unafanya ishindwe hata kusajili wachezaji wapya.

“Tunafanya zoezi hili kwa mujibu wa ripoti ya mwalimu, hatutaki kusajili kwa sababu tumesikia timu nyingine zinasajili. Tunafanya mambo yetu kimya kimya na mwisho wa siku wapenzi na wanachama wa Yanga watafurahi na roho zao,”amesema Mkwasa.

Katibu huyo amesema Yanga ina maeneo madogo tu ya kubadilisha na haihitaji kubadilisha timu nzima kama zinavyofanya timu nyingine.

Pamoja na hayo, Mkwasa amesema tayari wamekwishamalizana na wachezaji watatu wapya, lakini kwa sasa wataendelea kufanya siri.

“Tumekwishasajili wachezaji watatu wapya tumewapa mikataba tena kwa maridhiano na klabu zao, sasa tunasubiri muda ufike tuwatangaze,”amesema Mkwassa.

Mkwasa amesema hawataki kukurupuka kutangaza mchezaji kabla ya dirisha la usajili halijafunguliwa rasmi na wachezaji hao pia hawajamaliza kabisa mikataba na klabu zao, ili wasije kuadhibiwa tena.

“Sisi tunatakiwa kuwa makini kidogo, yasije yakatupata yaliyotupata kama ya Kessy (Hassan) kwa sababu tulipigwa faini Sh. Milioni 50 kwa kusajili mchezaji bado wiki moja tu amalize kabla mkataba wake,” amesema.

Mkwasa alikuwa anakumbushia usajili wa beki Hassan Kessy msimu uliopita kutoka kwa mahasimu, Simba SC ambao waliingia naye mkataba na kuanza kumtumia akiwa amebakiza wiki moja kumaliza kabisa mkataba wake na klabu yake ya zamani, hivyo mwisho wa siku Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) likawapiga faini ya Sh. Miliomi 50.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE →
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE →
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE →
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE →
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE →
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →