Idadi kubwa ya mashabiki wa Yanga wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kushuhudia mazoezi ya timu yao viwanja vya chuo cha Ualimu Butimba na Nyamagana
Uamuzi wa Yanga kuweka makazi kwa muda jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa kombe la Shirikisho, umefurahiwa na wengi
Pamoja na kuwa ugenini leo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc, hakuna shaka uwanja wa CCM Kirumba utazizima kwa shangwe za mashabiki wa Yanga, timu ya Mbao ndio itakayoonekana kama iko ugenini
Uongozi wa klabu ya Yanga umewashukuru mashabiki kwa kuendelea kuwaunga mkono tangu walipotua jijini Mwanza
Makamu Mwenyekiti Fredrick Mwakalebela amesema uungwaji mkono huo umeongeza morali ya wachezaji na benchi la ufundi na hivyo wana matumaini makubwa ya kushinda michezo yote miwili wakianza na Mbao Fc leo