Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inayohusishwa wachezaji wa ndani imefanikiwa kufuzu fainali za michuano ya CHAN baada ya kuichapa Sudan mabao 2-1 kwenye mchezo uliopigwa huko Sudan
Sudan ilitangulia kupata bao la kuongoza kwenye mchezo huo lakini mabao ya Erasto Nyoni na Ditram Nchimbi yalitosha kuihakikishia Stars ushindi muhimu kwenye kipindi cha pili
Tanzania imefuzu kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya timu hizo kufungana mabao 2-2 katika michezo yote miwili
Sudan ilishinda bao 1-0 kwenye mchezo uliopigwa jijini Dar es salaam lakini kwao wamefungwa mabao 2-1
Hii ni mara ya pili Stars itatinga fainali za michuano hiyo ambazo zitafanyika nchini Cameroon mwakani
Hongera Stars kwa kufuzu michuano hiyo...!
ADVERTISE HERE