Kiungo wa AS Kigali Haruna Niyonzima amesema yuko tayari kurejea kunako klabu yake ya zamani ya Yanga kama uongozi wa timu hiyo utamuhitaji
Juzi baada ya mchezo wa kirafiki kati ya Rwanda dhidi ya Tanzania, Niyonzima alikutana na Abdallah Bin-kleb Mjumbe wa Kamati ya usajili ya Yanga
Bin-kleb alikwenda Rwanda kwa majukumu ya timu ya Taifa akiwa mjumbe wa Kamati ya Uhamasishaji
Niyonzima alieleza furaha yake baada ya kukutana na Bin-kleb ambaye ndiye aliyesimamia usajili wake wakati anajiunga na Yanga mwaka 2012
Nahodha huyo wa Rwanda na AS Kigali, amesema hatakuwa na tatizo kurejea Yanga kwani ni klabu iliyomjengea jina na kupata mafanikio
"Kwanza nimefurahi kukutana na Bin Kleb kwa sababu yeye ni sawa na baba yangu kwa sababu ndiye ambaye alisimamia usajili wangu wakati ambao natua Tanzania kwa mara ya kwanza," amesema
"Lakini pia mimi sina ubaya na Yanga na nipo tayari hata leo kurudi na kuvaa jezi yao kama wakinihitaji kwa sababu naamini huko ni sehemu sahihi kwangu na ndipo nina upepo mzuri hapo, kitu cha muhimu wao waje kisha wazungumze nitakuwa tayari kwa ajili ya kujiunga nao"
Juzi Niyonzima aliupiga 'mpira mwingi' kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Stars ambayo ilimalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Nyota huyo aliyeitumikia Simba kwa misimu miwili kabla ya kuondoka msimu uliopita, anaonekana amerejesha makali yake
Inaelezwa alisaini mkataba wa miezi sita kuitumikia AS Kigali hivyo kama Yanga itamuhitaji inaweza kumsajili dirisha dogo akiwa mchezaji huru