Baadae leo Jumatano, Yanga itashuka uwanja wa Uhuru kumenyana na Pan African inayoshirki ligi daraja la kwanza
Mchezo huo ni mwendeleza ya mechi za kujipima nguvu wakati huu ambao ligi imesimama kupisha michezo ya kalenda za CAF na FIFA
Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema mchezo huo ni muhimu kwa ajili ya kuwaweka vijana wake sawa kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc ambao utapigwa Oktoba 22 kwenye uwanja wa CCM Kirumba
"Ligi imesimama kwa wiki tatu, ni muda mrefu kulikuwa na ulazima wa kucheza michezo ya kirafiki ili kuwaweka wachezaji katika ushindani"
"Jana (juzi) tumecheza na kesho (leo) tutacheza, mechi hizi pia zinatusaidia kuangalia mafanikio ya kile ambacho tumekuwa tukikifanya mazoezini," amsema
Baada ya mchezo huo Yanga itaelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu na kukamilisha maandalizi ya mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa Oktoba 27