Nyota waliokuwa majeruhi waongeza mzuka Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Oct 2019
Nyota waliokuwa majeruhi waongeza mzuka Yanga

Yanga imeanza kushusha presha baada ya wachezaji wake watano kurejea kazini tayari kujiandaa na mchezo dhidi ya Pyramid FC kwenye mechi ya mtoani kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Jana Yanga ilikuwa katika mazoezi na wakaialika Friends Rangers kama sehemu ya kujipima nguvu na kushinda mabao 4-2, huku David Molinga akifunga mara mbili huku mengine yakifungwa na nahodha wao Pappy Tshishimbi na mshambuliaji Maybin Kalengo katika ushindi huo.

Wakati Yanga ikiwa katika mchezo huo huku nje ya uwanja kulikuwa na mashine tano ambazo zilikuwa zikifanya mazoezi mepesi.

Mashine hizo ni mabeki Lamine Moro, Paul Godfrey ‘Boxer’ winga mkongwe Mrisho Ngassa, Patrick Sibomana na Sydney Urikhob ambao walikuwa majeruhi na sasa wameanza kurejea wakianza na mazoezi mepesi ya viungo.

Wachezaji hao ni kati ya 12 ambao walikuwa katika orodha ya wagonjwa na kuwapa wakati mgumu mabosi wa Jangwani ambao akili zao wamezielekeza kwenye mechi dhidi ya Pyramid.

Kocha Msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amesema kurejea kwa nyota hao kumepunguza presha ya benchi la ufundi na wanasubiri wachezaji hao kuwa fiti waweze kurejea na majukumu yao.

Amesema kurejea kwa wachezaji hao ni hatua nzuri na imewapa faraja kubwa wakati huu wakijipanga kumkabili Mwarabu mchezo ambao amesema utakuwa mgumu.

"Unajua hakuna kocha asiyefurahi kuona wachezaji waliokuwa majeruhi wanarejea, hii ni hatua kubwa hasa kwa idadi yao.

"Leo (jana) hawa watano wameanza na mazoezi mapesi na tunawafuatilia kwa karibu kuangalia uimara wao kama wataendelea kuimarika huku tukiwasubiri wengine, bado tuna muda wa kutosha kidogo kuweza kuwafuatilia,” Mwandila aliiambia Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’