CCM Kirumba itaturahisishia maandalizi - Mwakalebela

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Oct 2019
CCM Kirumba itaturahisishia maandalizi - Mwakalebela

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wameuchagua uwanja wa CCM Kirumba kuutumia mechi dhidi ya Pyramids Fc baada ya kujiridhisha unakidhi vigezo

Aidha Mwakalebela amesema Yanga inakabiliwa na mchezo wa ligi kuu mkoani Mwanza dhidi ya Mbao Fc hivyo wanaamini watakuwa na muda wa kujiandaa mkoani pamoja na kuzoea uwanja

"Tutakuwa Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi, hivyo Kamati ya Utendaji ikaona ni vyema mchezo dhidi ya Pyramids Fc tuupeleke huko kwani itaturahisishia maandalizi yetu," amesema

"Lakini tutakuwa na muda wa kutosha kuutumia na kuuzoea uwanja wa CCM Kirumba kabla ya kuwakabili Pyramids Oktoba 27"

"Muhimu zaidi tunawapa nafasi wakazi wa jiji la Mwanza na mikoa ya jirani kushuhudia mchezo wa Kimataifa baada ya kukosa burudani hiyo kwa miaka kadhaa"

Yanga inatarajiwa kuweka kambi ya wiki moja jijini Mwanza kabla ya mchezo huo

Aidha, mabingwa hao wa kihistoria watautumia mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc ambao utapigwa Oktoba 24 kama sehemu ya maandalizi yao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
8h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
16h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
19h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’