Kamati ya Ufundi ya klabu ya Yanga imeeleza kuwa na imani na kocha Mwinyi Zahera hivyo kutaka apewe muda wa kuijenge timu
Yanga imenza vibaya msimu wa ligi kuu ya Vodacom ikishinda mchezo mmoja, kutoka sare na kufungwa mchezo mmoja
Hata hivyo Kamati hiyo imesema bado ni mapema sana kumhukumu Zahera kwa matokeo ya michezo hiyo
Mwenyekiti wa kamati Salum Rupia amesema wanaamini Zahera ataweza kuiweka sawa Yanga na kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya kombe la Shirikisho
"Tuna imani na Zahera licha ya kuyumba katika mechi chache, kwani anaendelea kufanyia kazi mapungufu yanayojitokeza," amesema
Naye Katibu Mkuu wa Kamati hiyo Charles Mkwasa amesema michezo mitatu haitoshi kusema kuwa timu imefanya vibaya kwenye ligi
"Ni mapema sana kukata tamaa, kwa kuwa hata nusu ya mechi za Ligi Kuu hazijachezwa hivyo wakati wa kuona timu imefanya vibaya si sasa," amesema
Aidha Kamati hiyo imeahidi kuendelea kushirikiana na Zahera na benchi lake la ufundi kuhakikisha timu inafanya vizuri