Yanga imebadili maisha yangu - Metacha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Oct 2019
Yanga imebadili maisha yangu - Metacha

Mlinda lango wa Yanga Metacha Mnata amekiri kuwa tangu ajiunge na timu hiyo amepata mafanikio katika kipindi cha muda mfupi jambo ambalo hakuwahi kulipata katika timu alizocheza mwanzo

Metacha alitua Yanga usajili uliopita akitokea klabu ya Azam Fc

Msimu uliopita aliitumikia Mbao Fc kwa mkopo

Mlinda lango huyo ambaye yuko timu ya Taifa, amesema licha ya presha kubwa anayoipata katika klabu ya Yanga kutokana na timu hiyo kuhitaji matokeo ya ushindi kwenye kila mchezo, Yanga imebadili maisha yake kutoka mtu wa kawaida na kuwa mtu maarufu

"Hii ni mara ya kwanza kwangu kucheza Yanga ni klabu kubwa, ina presha tofauti na timu nilizopitia kwa maana ya Azam FC na Mbao FC ambako mchezaji huwezi kuwa katika mawazo makubwa kama huku, lakini nimeanza kunufaika," Mnata amenukuliwa na Mwanaspoti

"Kupitia kujulikana najikuta baadhi ya mambo yangu ya kimaisha yanakwenda, hilo ni jambo linaloendelea kunipa moyo wa kupambana kuamini siku moja nitakuwa mtu wa tofauti katika soka la Tanzania"

Metacha amejiwekea malengo ya kupata mafanikio zaidi msimu huu licha ya kukabiliwa na ushindani mkali wa namba kutoka kwa mlinda lango wa Kimataifa wa Kenya, Farouk Shikalo

"Ugumu wa kazi ndio unaomtambulisha mtu kuwa bora, naendelea kujituma na kujifunza kwa wale ambao wamenitangulia kwa uzoefu, naamini utakuwa mzuri kwa upande wangu kutoka hatua moja kwenda nyingine"

Metacha ni miongoni mwa wachezaji wanne wa Yanga walioitwa timu ya Taifa inayojiandaa na mchezo wa Kimataifa wa kirafiki dhidi ya Rwanda ambao utapigwa Oktoba 14

Baadae wataelekea Uganda ambapo Oktoba 18 wataikabili Sudan kwenye mchezo wa marudiano kusaka tiketi ya michuano ya CHAN

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’