Matokeo ya mechi ya Yanga vs Coastal Union hayatabadilika - Ten

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Oct 2019
Matokeo ya mechi ya Yanga vs Coastal Union hayatabadilika - Ten

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema matokeo ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom baina ya timu yake dhidi ya Coastal Union hayatabadilika na kuwa mjadala wa uhalali wa goli la Yanga hauwezi kubadili chochote

Jana Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Uhuru

Bao la kiungo Abdulaziz Makame liliibua mjadala mkali kwenye mitandao ya kijamii huku baadhi ya mashabiki wakimtupia lawama mwamuzi kwa kulikubali bao hilo wakidai mlinzi wa Coastal Union aliokoa mpira kabla haujavuka mstari

Lakini uchambuzi wa picha za marudio unaonyesha mlinzi huyo alikuwa amevuka mstari sambamba na mpira wakati akiokoa

Aidha kulikuwa na mkanganyiko kati ya Mwamuzi wa kati na msaidizi wake ambapo mwamuzi wa pembeni aliinua kibendera akiashiria mfungaji alikuwa ameotea

"Tunaandika tu ujumbe, watakaosoma watawafikishia wahusika, Yanga 1-0 Coastal Union mechi iliisha hivyo haitabadilika. Msimalize bando kuposti video," ameandika Ten kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram

Pamoja na utata wa bao hilo, mshambuliaji David Molinga alifunga bao kwenye dakika ya 81 lakini lilikataliwa na mwamuzi msaidizi akidhania kuwa alikuwa amepotea

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’