FT : Yanga 3-3 Polisi Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Oct 2019
FT : Yanga 3-3 Polisi Tanzania

Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Yanga dhidi ya Polisi Tanzania umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kutoka sare ya mabao 3-3

Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Uhuru, uliishuhudia Yanga ikilazimika kutokea nyuma kwa mabao mawili na kupata sare hiyo

Yanga iliuanza mchezo huo kwa kasi na iliandika bao la kuongoza mapema tu kwenye dakika ya 6 kupitia kwa Mrisho Ngasa aliyemalizia krosi murua ya Juma Abdul

Baada ya kufunga bao hilo, Yanga ilipunguza kasi na kuwapa nafasi wapinzani wao kutawala mchezo

Ditram Nchimbi akaisawazishia Polisi kwenye dakika ya 34 baada ya kuuwahi mpira uliokuwa ukielea langoni kwa Yanga

Katika kipindi cha pili, uzembe wa mabeki ukaruhusu Nchimbi afunge mabao mengine mawili ya haraka haraka kwenye dakika za 55 na 58

Kuingia kwa mabao hayo kuliiamsha Yanga ambayo ililishambulia mfululizo lango la Polisi

Mcongomani David Molinga 'Falcao' ambaye alikosa nafasi ya wazi kwenye kipindi cha kwanza, akafungua akaunti yake ya mabao akifunga bao la kichwa kwenye dakika ya 65

Dakika tatu baadae, Molinga akafunga bao safi kupitia mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja kimiani

Matokeo ya mchezo huo yanaifanya Yanga iambulie alama moja tu baada ya kushuka dimbani mara mbili

Yanga itashuka tena uwanja wa Uhuru Jumapili, kuikabili Coastal Union

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’