Wakati mchezo ukielekea ukingoni huku Yanga ikiwa nyuma kwa mabao 2-1, kocha Mwinyi Zahera alitaka kufanya mabadiliko kwa kumtoa Sadney Urikhob ili kumuingiza Maybin Kalengo
Hata hivyo beki Lamine Moro alipinga mabadiliko hayo hali iliyomfanya Zahera amtoe beki Ally Ally ambaye alionekana kuchoka dakika za majeruhi
Lamine alitolewa kwa kadi nyekundu dakika chache baadae baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano
Lakini tukio hilo kinadhihirisha ujasiri wake. Ni mchezaji anayejituma sana uwanjani na wakati wote anapambana ili kuipa timu mafanikio
Lamine aliona Yanga iliyokuwa ikisaka bao la kusawazisha, bado ilimuhitaji Sadney ambaye ndiye aliyefunga bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo
Kwa hiyo haikuwa sahihi kumtoa mshambuliaji huyo ambaye tayari alikuwa ana kasi ya mchezo
Ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, ilikuwa sahihi kutoa beki kuingiza mshambuliaji
Katika dakika za majeruhi Zesco walikuwa wakijihami zaidi kulinda ushindi wao wakati kwa Yanga walikuwa wanahitaji bao la kusawazisha
Kusingekuwa na cha kupoteza hata kama Yanga ingefungwa bao jingine