Sare ya Dar imewabeba Zesco makundi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Sep 2019
Sare ya Dar imewabeba Zesco makundi

Pamoja na kupoteza mchezo dhidi ya Zesco, wachezaji wa Yanga wameonyesha ujasiri mkubwa wa kupambana katika mchezo huo uliokuwa mgumu

Kujifunga kwa Makame ni tukio la bahati mbaya hivyo hawezi kulaumiwa kwa kuwa ni sehemu ya mchezo

Jambo pekee la kujilaumu ni kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa nyumbani

Kwani kama Yanga ingeshinda mchezo wa kwanza hata kwa bao 1-0, ingeweza kutinga makundi licha ya kupoteza mchezo wa leo

Hili ni jambo ambalo benchi la ufundi linapaswa kulifanyia kazi ili kuhakikisha Yanga inashinda inapocheza nyumbani

Kutolewa kwa Yanga leo kumesababishwa na sare ya bao 1-1 ya mchezo wa kwanza

Timu inaelekea kwenye michuano ya kombe la Shirikisho ambako itapangwa na moja ya timu zitakazofuzu hatua ya 16 bora kwenye michuano hiyo

Mchezo wa kwanza Yanga itakuwa nyumbani. Ushindi katika mchezo huo ni lazima ili kupunguza presha ya mchezo wa marudiano

Safu ulinzi ya Yanga pamoja na mlinda lango Metacha Mnata leo walifanya kazi kubwa kuhakikisha timu inapata matokeo

Makosa madogo tu yamewanufaisha Zesco lakini zaidi yamechangiwa na sare ya mchezo wa kwanza

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’