Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka keshokutwa Jumanne, Septemba 24 kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Zesco United
Mchezo huo utapigwa Septemba 28 katika uwanja wa Levy Mwanawasa jijini Ndola
Yanga itaondoka ikiwa na kikosi chake kamili kitakachowajumuisha nyota wake walioitwa timu ya Taifa ambao leo watakuwa uwanja wa Taifa kuikabili Sudan
Yanga itaweka kambi ya siku tano Zambia kabla ya kuwakabili wenyeji wao siku ya Jumamosi huku wakihitaji ushindi au sare ya kuanzia mabao mawili ili waweze kusonga mbele
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema mpaka sasa ni Paulo Godfrey 'Boxer' ndiye hana uhakika wa kusafiri na timu nchini Zambia kwa kuwa bado ni majeruhi
Amesema orodha ya kikosi kitakachosafiri itatolewa baadae