Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema katika kikosi chake anataka wachezaji wawe na uzito sahihi ili kuweza kutimiza majukumu yao vyema
Baada ya kufanya kazi ya kumpunguza uzito mshambuliaji David Molinga, zoezi hilo limehamia kwa Mganda Juma Balinya
Balinya hakucheza mechi dhidi ya Zesco United, Zahera amefichua kuwa Mganda huyo hakuwa tayari kwa mchezo
"Balinya aliongezeka kilo nne, tulipokuwa Mwanza tulimpa program maalum ya kupunguza uzito, alipungua kilo mbili"
"Kabla ya mechi ya marudiano na Zesco atakuwa sawa na pengine tutamtumia," amesema Zahera
Balinya ndiye aliyeipeleka Yanga raundi ya kwanza akiifunga bao la ushindi dhidi ya Township Rollers nchini Botswana
Balinya na Molinga sio wachezaji wa kwanza kutakiwa kupunguza uzito na kocha Zahera
Beki Juma Abdul nae aliwahi kukumbana na zoezi hilo