Lwandamina anaujua mziki wa Yanga ugenini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Sep 2019
Lwandamina anaujua mziki wa Yanga ugenini

Kocha Mkuu wa ZESCO United George Lwandamina amesema anafahamu mchezo wa marudiano kati ya timu yake dhidi ya Yanga utakaopigwa nchini Zambia hautakuwa mwepesi kutokana na rekodi za timu hizo

ZESCO itakuwa mwenyeji wa mchezo huo utakaopigwa Septemba 26 nchini Zambia

Yanga imekuwa na mwenendo mzuri wa matokeo inapocheza ugenini kuliko nyumbani

Tayari imedhihirisha hilo katika mchezo wa hatua ya awali kwa kuichapa Township Rollers bao 1-0 nchini Botswana baada ya sare ya bao 1-1 katika mchezo uliopigwa Dar

Lwandamina amesema anafahamu rekodi hiyo kwani hata wakati akiwa na Yanga walifanya vizuri zaidi katika michezo ya Kimataifa waliyocheza ugenini

Lakini amesema ZESCO pia ina rekodi ya kutofungwa inapocheza uwanja wa nyumbani

"Najua Yanga ina takwimu nzuri katika michezo ya ugenini, hata wakati wa kipindi changu, lakini Zesco nayo haijawahi kufungwa mechi yoyote ya Kimataifa Zambia"

"Utakuwa ni mchezo mgumu lakini tutakuwa na nafasi zaidi ya kutumia vyema uwanja wa nyumbani"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’