Uongozi wa Klabu ya Yanga, Mwenyekiti Dr. Mshindo Msolla, Makamu wake Fredrick Mwakalebela na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wanatoa pongezi nyingi kwa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, wachezaji wote, benchi na ufindi na kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ushindi dhidi ya Burundi ulioiwezesha Tanzania kusonga mbele hatua ya makundi ya Kombe la Dunia kwa nchi za Afrika
Uongozi wa Yanga unaamini kwamba mafanikio haya ni hatua moja kubwa katika kukua kwa soka la Tanzania, na hivyo kuwahimiza Watanzania na Wanamichezo wote kuendeleza umoja, amani na mshikamano michezoni ili kuleta mafanikio katika soka la Tanzania
Tanzania imesongaa mbele kwa ushindi wa jumla wa mikwaju ya penati 3-0 baada ya michezo miwili baina ya timu hizo kumalizika kwa sare ya bao 1-1