Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema wameipokea leseni ya mlinda lango Farouk Shikalo kutoka Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF)
Shikalo sasa anaweza kucheza mechi dhidi ya ZESCO United, uamuzi ukibaki kwa kocha Mwinyi Zahera na benchi lake la ufundi
Hata hivyo Mwakalebela amesema leseni za David Molinga na Mustafa Suleyman bado wanaendelea kuzifuatilia
Wachezaji hao hawakuwa sehemu ya kikosi kilichoiondosha Township Rollers kwenye mchezo wa hatua ya awali
Wakati Molinga hakuandikishwa kwa wakati kutokana na usajili wake kuchelewa, beki Mustafa Suleyman yeye ITC yake ilichelewa
ADVERTISE HERE