Yanga haisajili timu nzima

Admin By Admin
β€’
25 Jun 2017
Yanga haisajili timu nzima
Kumekuwa na hofu kubwa kwa mashabiki wa Yanga kwenye kipindi hiki cha usajili wengi wakiamini timu yao haifanyi vizuri katika usajili.

Wengi wamekuwa wakiangalia upande wa wapinzani, Simba ambao wanaonekana kusajili asubuhi, mchana na jioni.

WanaYanga hawapaswi kuingia hofu kwa kuangalia upande wa wapinzani kwani kila timu ina mipango yake.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwassa alishaliweka wazi hilo kuwa Yanga haisajili timu nzima, inafanya usajili wa marekebisho madogo tu.

Usajili wa Yanga unafanywa kulingana na mapendekezo ya kocha George Lwandamina ambaye aliagiza asajiliwe mshambuliaji wa nguvu, mfungaji wa magoli, mwenye maamuzi ya haraka, mwenye kujiamini na mpira, anayeweza kutumia miguu yote.

Pia kiungo mkabaji, beki wa kati anayetumia miguu yote, kiungo wa kushoto na beki wa kushoto.

Baadhi ya wachezaji tayari wameshapatikana. Kwenye sehemu ya kiungo Pius Buswita na Raphael Daudi wanakidhi vigezo vya kocha Lwandamina.

Abdallah Hajji Γ’β‚¬ΛœNinjaÒ€ℒ ni beki wa kati, Yanga haijakurupuka kumnasa beki huyu kutoka Taifa ya Jan'gombe.

Kwa mshambuliaji hakuna mtu mwenye shaka juu ya uwezo wa Ibrahim Ajib Migomba na ni miongoni mwa sajili zitakazoleta manufaa Jangwani.

Yanga imemnasa pia mlinzi wa kushoto Gardiel Michael kutoka Azam FC na iko mbioni kusajili beki mwingine wa kati pamoja na mshambuliaji.

Simba ni kawaida yao kusajili timu nzima karibu kila msimu katika misimu mitatu iliyopita.

Yanga imetwaa ubingwa wa VPL kwa misimu mitatu mfululizo na hakukuwa na marekebisho makubwa sana katika kikosi.

Cha muhimu ni mashabiki kutulia kuuachia uongozi ufanye kazi yake. Uongozi ukishakamilisha usajili utatoa taarifa iliyokamilika.

Ipo changamoto kwa baadhi ya wachezaji ambao mikataba yao imemalizika wengine wanadai pesa zaidi ili waongezewe mikataba lakini naamini kwa wale wenye umuhimu Yanga itawabakisha kwa gharama yoyote.

Fahamuni kutwaa ubingwa misimu mitatu mfululizo na mwingine kukosa ubingwa misimu mitano mfululizo sio mambo mepesi.

Simba inafanya usajili 'mpya' ikiamini inajenga timu imara kwa ajili ya kutwaa ubingwa msimu ujao lakini pia inaihofia Yanga ndio maana Simba iko tayari kuwanunua wachezaji wote muhimu wa Yanga hata kama hawatawatumia lengo likiwa kuidhoofisha Yanga.

Huko kwenye vyombo vya habari ndio kabisaa, vingine vimenunuliwa ili viandike habari za uongo kuhusu Yanga hasa masuala ya fedha ili kuwafanya wachezaji wazuri wanaowaniwa na Yanga wakatae kujiunga kwa kuhofia ukata unaohubiriwa na magazeti flani flani.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
6h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
18h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’