Beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani, amesema timu hiyo kwa sasa ina safu bora ya ulinzi ukilinganisha kipindi cha misimu miwili iliyopita
Tangu kuondoka kwa beki Vicent Bossue na baadae kustaafu Nadir Haroub, safu ya ulinzi ya Yanga iliyumba
Hata hivyo baada ya usajili wa wachezaji wapya, Yondani anasema ukuta wa Yanga umeimarika

"Ukiangalia kiwango cha mchezaji mmoja mmoja, kwa maana ya Lamine, Godfrey na Sonso, ukigeukia kwa makipa, tuna kijana mdogo Metacha pamoja na Shikalo, wote wanayajua majukumu yao," amesema
"Kwa muda mfupi na mechi tulizocheza, nafurahishwa na aina ya uchezaji wa mabeki katika zoezi la kuokoa mipira na kupunguza hatari langoni, hili linanipa faraja kuwa tuna uwezo wa kupata matokeo mazuri katika mashindano tunayocheza"
"Hata kama mmoja wapo akikosekana, tuna uhakika waliokuwepo watatimiza majukumu yao vizuri. Msimu huu unaweza kuwa ni wa tofauti kwa Yanga hata kama tumeanza kwa kupoteza mechi ya ligi"
Walinzi wapya walioongezwa kwenye kikosi cha Yanga ni pamoja na Ally Ally, Ally Mtoni, Lamine Moro, Mustafa Suleyman na Muharami Issa 'Marcelo'