Wakati ikisubiri kuelekea jijini Mwanza kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa, Yanga imeendelea kujifua uwanja wa Chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es salaam
Moja ya changamoto zinazoikabili Yanga sasa ni safu yake ya ushambuliaji kukosa makali
Kwa takribani siku mbili, Zahera ametilia mkazo safu hiyo
Mshambuliaji David Molinga 'Falcao' huenda akapewa jukumu la kuwa mshambuliaji kiongozi mechi dhidi ya ZESCO
Molinga ameonyesha utofauti tangu aanze kupewa nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Yanga ina uhakika wa kumtumia kwenye mechi zijazo za ligi ya mabingwa kwa kuwa ameshapata kibali kutoka CAF
Molinga amekuwa akicheza sambamba na Sibomana, Sadney na Balinya
Hata hivyo Sibomana anatarajiwa kuelekea Rwanda kujiunga na timu ya Taifa
Kocha Mwinyi Zahera ana siku 13 za kukiandaa kikosi chake tayari kwa mchezo wa kwanza dhidi ya ZESCO ambao utapigwa Septemba 14 kwenye uwanja wa taifa