Mwakalebela asifiwa kwa kuandaa mazingira ya ushindi Botswana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Aug 2019
Mwakalebela asifiwa kwa kuandaa mazingira ya ushindi Botswana

Imeelezwa kuwa ushindi wa Yanga nchini Botswana ulichangiwa na mambo mengi, ikiwamo kitendo cha Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela kuwazidi ujanja wenyeji wao.

Mmoja wa Watanzania wanaoishi Botswana, Dickson John, aliliambia gazeti la Bingwa kuwa viongozi wa Township Rollers walitishwa na kocha wao, Tomas Trucha, raia wa Jamhuri ya Czech alipowaambia Yanga si timu ya mchezo mchezo hivyo kusuka mikakati kabambe ya nje ya uwanja ili kuwamaliza Wanajangwani hao.

"Walipanga kuwaanza kuwadhibiti Yanga toka uwanja wa ndege hadi hotelini, waliposikia kuna viongozi wa Yanga walishatangulia hapa, walipagawa, wakahofu mambo yao yasijejulikana na kujitia aibu CAF (Shirikisho la Soka Afrika), matokeo yake wakaamua kusubiri matokeo ya uwanjani," alisema.

Watanzania waishio Botswana walikuwa na mchango mkubwa kwani walihaha kushirikiana na Mwakalebela na viongozi wengine wa Yanga kuhakikisha hakuna hujuma yoyote inayofanyiwa timu yao na mwisho wa siku, mshindi apatikane uwanjani kama ilivyokuwa.

"Jana (juzi) baada ya mchezo, viongozi wa Rollers na mashabiki wao, walichanganyikiwa, hawakuamini kilichotokea," alisema John.

Yanga haikumpeleka Mwakalebela Botswana kwa bahati mbaya, uzoefu wake kwenye masuala ya Kimataifa kufahamiana na watu nchini Botswana ilikuwa ni faidi kubwa kwa Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’