FT : Yanga 0-0 Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Oct 2017
FT : Yanga 0-0 Mtibwa Sugar
Mchezo wa ligi kuu ya Vodacom kati ya Yanga dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye dimba ka Uhuru umemalizika kwa suluhu ya 0-0.

Licha ya kutawala mchezo huo kwa muda mwingi hasa kipindi cha pili, washambuliaji wa Yanga walishindwa kuukwamisha mpira wavuni.

Katika mchezo huo Yanga ilimtumia kiungo Pius Buswita kwa mara ya kwanza msimu huu baada ya kumaliza utata wa usajili wake, amecheza vizuri.

Safu ya ushambuliaji ya Yanga ilichangamka zaidi kwenye kipindi cha pili baada ya kocha George Lwandamina kuwaingiza Thabani Kamusoko, Geofrey Mwashiuya na baadae Juma Mahadhi kuchukua nafasi za Chirwa, Raphael Daudi na Donald Ngoma aliyepata majeraha.



Uimara wa mlinda lango wa Mtibwa Benedict Tinocco uliinyima Yanga nafasi ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

Mtibwa Sugar nao hawakuwa nyuma kwenye mchezo huo kwani waliweza kutengeneza mashamulizi kadhaa kupitia kwa mshambuliaji wake Stamili Mbonde lakini uimara wa safu ya ulinzi wa Yanga na mlinda lango Youthe Rostand, ilikuwa kikwazo kwao.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga ishindwe kuibuka na ushindi katika mchezo wa tatu kati ya mitano iliyocheza.

Aidha hiyo ni sare ya pili kwa mabingwa hao watetezi kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Licha ya matokeo hayo Mtibwa Sugar imeendelea kuwa kileleni baada ya kufikisha alama 11 sawa na Azam FC iliyotoka sare ya bao 1-1 na Singida United.

Simba ina nafasi ya kukwea kileleni mwa msimamo wa ligi kama itapata ushindi dhidi ya Stand United kesho Jumapili.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’