Mshambuliaji mpya wa Yanga David Molinga leo amepata nafasi ya kucheza kwa dakika 90 mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania
Mcongomani huyo aliongoza safu ya ushambuliaji akiwa pekee mbele akisaidiana na Deus Kaseke/Bigirimana na Kalengo waliotokea pembeni
Kwenye mchezo huo ambao Yanga ilikubali kipigo cha mabao 2-0, safu ya ushambuliaji haikuwa na maelewano mazuri hivyo kumfanya Molinga mara kwa mara atokeo katika nafasi yake kusaka mipira
Ameonyesha kiwango cha kuridhisha na huenda atakapojumuishwa kwenye kikosi cha kwanza, anaweza kuwa na mchango zaidi
Licha ya mwili wake mkubwa, ni mwepesi, ana nguvu na kasi
ADVERTISE HERE