Zahera 'achekelea' Abdul kurejea Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Aug 2019
Zahera 'achekelea' Abdul kurejea Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kurejea kwa beki Juma Abdul ni habari njema kwa kikosi chake kinachojiandaa na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers

Abdul alikosa mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam, akiweka ngumu kuingia kambini hadi alipwe madai yake

Abdul ana nafasi ya kuanza mchezo utakaopigwa Botswana August 23 baada ya Boxer kupata majeraha

Zahera amefichua kuwa anataka kumtumia Abdul kwenye mechi hiyo ya ugenini kumimina krosi zenye macho ambazo zitakuwa zikiwafikia mastraika wake watakaokuwa na kazi ya kufunga tu, baada ya kubaini kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita walizikosa krosi hizo.

"Kikosi chetu kilikuwa kikimtegemea zaidi Boxer ambaye atakuwa nje kwa muda baada ya kuumia goti kwenye mchezo wa awali ulioisha kwa sare ya 1-1, lakini hata wale ambao niliwatumia kuziba nafasi yake hawakufiti ndio maana nimefurahi Abdul kurejea," Zahera amenukuliwa na Mwanaspoti

Zahera alisema kwa jinsi alivyowasoma wapinzani wake amegundua ni wabovu kwenye mipira ya krosi, hivyo ujio wa beki huyo anayefanya vizuri eneo hilo inaweza ikawa dawa dhidi ya wapinzani wao kuweza kupata matokeo katika uwanja wao wa ugenini

Kuhusu Yondani, Zahera alisema pia ana nafasi ya kucheza itategemea na mfumo atakaoutumia, huku akiwamwagia sifa mabeki Ally Mtoni β€˜Sonso’, Lamine Moro jinsi walivyocheza kwa kuelewana hawakuwa na makosa mengi kwenye mchezo huo.

Alisema kwa mfumo wa kuchezesha mabeki watatu Yondani anaweza kufiti kwa kukaa kati huku Sonso na Moro wakiwa pembeni yake, lakini alisisitiza mchezo unaofuata unahitaji mawinga wenye kasi sambamba na mabeki wa kupanda kupitia pembeni.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’