Zahera kuzitumia Polisi Tanzania, AFC Leopards kuboresha kikosi

Selemani Sudi By Selemani Sudi
β€’
13 Aug 2019
Zahera kuzitumia Polisi Tanzania, AFC Leopards kuboresha kikosi

Moja ya changamoto ambayo iliikabili Yanga kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Rollers, ni kukosa maelewano mazuri hasa kwa safu yake ya ushambuliaji inayoundwa na wachezaji wote wageni

Sababu inayotajwa kupelekea changamoto hiyo ni wachezaji hao kutofanya mazoezi pamoja kwa muda wa kutosha

Wachambuzi mbalimbali wa soka nchini wanaamini kama Yanga ingepata muda mrefu zaidi wa kufanya mazoezi pamoja, mechi ya juzi dhidi ya Rollers ingekuwa nyepesi kwao

Changamoto hiyo aliidokezea hata kocha Mwinyi Zahera baada ya mchezo wa wiki ya Mwananchi dhidi ya Kariobangi Sharks

Zahera alisema timu yake haina muunganiko mzuri kutokana na wachezaji kutoanza mazoezi pamoja

Mcongomani huyo ndio maana ametaka apate michezo zaidi ya kirafiki ili aweze kutengeneza muunganiko huo

Michezo miwili dhidi ya Polisi Tanzania na AFC Leoprads ni kipimo cha kazi anayoifanya Zahera kwenye viunga vya mazoezi

Lakini pengine hili lilipaswa kufanywa mapema kwani ilifahamika wingi wa wachezaji wapya, timu ingehitaji muda zaidi wa maandalizi

Muingiliano wa ratiba ya michuano ya Afcon kwa kiasi kikubwa imevuruga mipango ya mazoezi ya timu nyingi ikiwemo Yanga

Lakini pia ni wakati sasa kwa uongozi wa Yanga kumuondolea Zahera majukumu ya timu ya Taifa, ili abaki na jukumu moja tu la kuifundisha Yanga

Ingawa kocha Mkuu wa DR Congo Florent Ibenge amejiuzulu, bado hatma ya Zahera kama kocha Msaidizi haijawekwa wazi na chama cha soka cha DRC

Uongozi wa Yanga unapaswa ukae nae chini, ili makubaliano yafikiwe aamue kubaki na majukumu ya Yanga tu hata kama ikitokea ametakiwa kuendelea na majukumu hayo ya timu ya Taifa

Kwani athari za kukosekana kwake hata kama ni wiki moja ni kubwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
35m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’