Kukosa penati kuliniondoa mchezoni - Sibomana

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Aug 2019
Kukosa penati kuliniondoa mchezoni - Sibomana

Mshambuliaji wa Yanga Patrick Sibomana amefichua kuwa mkwaju wa penati aliokosa kwenye dakika ya 30 ya mchezo dhidi ya Township Rollers, ulimuondoa mchezoni kwa muda

Sibomana mmoja wa wapambanaji wapya kwenye kikosi cha Yanga amesema walihitaji kushinda mchezo huo hivyo aliumia sana baada ya kukosa mkwaju wa penati

"Ilikuwa nafasi adimu kwetu, baada ya kukosa nilisikitika sana, nilikuwa nikifikiria nitawaambia nini wachezaji wenzangu na mashabiki wetu," alisema

Hata hivyo Sibomana amesema kuwa alijipa moyo na kuendelea kuipigania timu

Kuhusu kupiga penati ya pili, Sibomana amefichua awali alimtaka nahodha Papi Tshishimbi apige lakini akamwambia apige tena

"Nilimwambia Tshishimbi apige lakini naye akaniruhusu nipige tena"

Sibomana amesema wanajiandaa kikamilifu kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Botswana August 25

"Bado tuna nafasi ya kusonga mbele, sasa tunajiandaa vyema kuweza kupata matokeo ugenini"

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’