Abdul bado anahitajika sana Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Aug 2019
Abdul bado anahitajika sana Yanga

Juzi baada ya kuumia Paulo Godfrey 'Boxer', kocha Mwinyi Zahera alilazimika kumuingiza Ally Ally kuchukua nafasi yake

Licha ya kufanya vizuri katika ulinzi, Ally Ally alikosa ubunifu kwenye ushambuliaji

Mipira yake mingi ya krosi ilitoka nje au iliishia mikononi mwa mlinda lango

Ulikuwa ni wakati ambao mashabiki walimkumbuka beki Juma Abdul ambaye hakuwa na timu

Abdul na Andrew Vicent hawakuingia kambini mkoani Morogoro kutokana na mgogoro uliokuwepo kati yao na uongozi

Lakini hapana shaka kama Abdul angekuwepo mechi ya juzi, krosi zake zingesababisha madhara zaidi langoni kwa Rollers

Walinzi wa Rollers walionyesha udhaifu katika kucheza mipira ya krosi

Mikwaju yote miwili ya penati yalikuwa matokeo ya mipira hiyo

Hapana shaka wiki mbili kabla ya mchezo wa marudiano zinatosha kumuimarisha Abdul ili aweze kuwa na mchango kwenye mchezo huo

Ili kupata matokeo Botswana, Yanga itapaswa kucheza kama ilivyocheza kipindi cha pili juzi kwa kupitia pembeni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
4h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
9h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’