Timu ya hamasa Yanga ijipange

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Aug 2019
Timu ya hamasa Yanga ijipange

Idadi ya mashabiki waliojitokeza uwanja wa Taifa leo kuiunga mkono Yanga dhidi ya Township Rollers haikuwa ya kuridhisha

Kwa kiwango kilichoonyeshwa na Yanga leo, kama mashabiki wangejaa kama siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi, hakika timu ingeweza kufanya vizuri zaidi

Wingi wa mashabiki uwanjani ni silaha muhimu michezo ya nyumbani

Watani zetu Simba msimu uliopita walifanikiwa michezo yao yote ya nyumbani sio kwa kuwa walikuwa na kikosi imara sana, hapana, bali walitumia michezo ya nyumbani kuwafunga wapinzani wao kisaikolojia kabla ya mchezo

Kwani kitendo cha wageni kuingia uwanjani na kukuta mashabiki wametapakaa, kinawaweka kwenye hofu

Pengine kitengo cha uhamasishaji klabu ya Yanga kinapaswa kubadili mbinu ili kuwashawishi mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kwenye michezo kama hii

Mahudhurio hafifu ya mashabiki yanaweza kushusha morali ya wachezaji

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’