Zahera ataja sababu ya kumsajili Molinga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Aug 2019
Zahera ataja sababu ya kumsajili Molinga

Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera, ameweka wazi sababu ya kumsajili mshambuliaji David Molinga Ndama ‘Falcao’ katika kikosi chake.

Usajili wa mchezaji huyo ulifanyika nyakati za mwisho -tena kwa kumkata kipa Klaus Kindoki na ndipo Falcao akatua katika kikosi hiko.

Zahera amesema katika usajili wake alisajili mshambuliaji mmoja tu (Sadney) ambaye kazi yake ni kutupia nyavuni hivyo ilimlazimu kuongeza mtu mwingine.

"Sina washambuliaji wengi, nina Sadney na huyu Falcao. Balinya ni namba kumi lakini anaweza kucheza kama kiungo ni sawa na Kalengo ambaye ni winga licha ya kuweza kucheza kama mshambuliaji," Zahera aliliambia Mwanaspoti

Akizungumzia uwezo wa Falcao alisema katika msimu uliopita alikosa mtu ambaye alikuwa na spidi na uwezo wa kupambana, ndio maana ameamua kumsajili Falcao

"Mara kwa mara nilikuwa namwambia (Herietier) Makambo kuwa licha kufunga lakini hana spidi, hakuwa mtu wa kupiga chenga na kwenda kufunga ndio maana nimemleta Falcao, nilikuwa namwambia hata yeye"

Alisema katika upande wa spidi nyota huyo mpya ana kasi na ndio jambo ambalo alikuwa analiangalia katika usajili wake mpya.

"Falcao anajua kufunga, kupambana na spidi. Kwa hiyo naamini atafanya vizuri, kwa upande wa mawinga pia kuna wachezaji wapya ambao wana kasi na wanajua kupiga krosi sahihi, hivyo, hakuna wasiwasi," alisema.

Aliongeza kuwa mpira wake ni wa mbio, mshambuliaji wake Falcao ana uwezo huo huku Sadney akiwa na uwezo mkubwa wa kumtoka beki pindi wanapokuwa pamoja.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
33m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’