Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema beki kisiki wa timu hiyo Kelvin Yondani ataungana nao watakaporejea jijini Dar es salaam
Yanga itarejea Dar kesho Ijumaa tayari kwa mchezo dhidi ya Township Rollers utakaopigwa Jumamosi, August 10 kwenye uwanja wa Taifa
Akizungumza jana baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege Fc, Zahera alisema mkongwe huyo alimuomba ruhusa apumzike baada ya kurejea kutoka Kenya alikokuwa na majukumu ya timu ya Taifa
"Yondani ataungana na sisi, tukirejea Dar ataanza mazoezi" amesema
"Baada ya kutoka Kenya aliniomba apumzike, nami nimemruhusu"
Kuhusu mabeki Juma Abdul na Andrew Vicent Zahera amesema walinzi hao watajiunga kambini wakati wowote baada ya kumaliza na uongozi wa Yanga kuhusu madai yao
"Sina tatizo na Abdul na Dante.. Nlisimulia nao na tukakubaliana watajiunga nasi baada ya changamoto zao kutatuliwa"
Licha ya kukosekana kwa wachezaji hao, Zahera ameonyesha kutokuwa na wasiwasi kutokana na upana wa kikosi chake
Yanga imeongeza walinzi wanne wa kati Lamine Moro, Ally Mtoni, Ally Ally na Mustafa Suleyman ambao wote wako katika kiwango bora
Moro na Mtoni wanaonekana kuwa chaguo la kwanza kwani walicheza mchezo dhidi ya Sharks na jana wakaanza pamoja mchezo dhidi ya Mlandege Fc lakini kwenye kipindi cha pili wakatoka nafasi zao zikichukuliwa na Ally Ally na Mustafa Suleyman