Kikosi cha Yanga kitarejea tena dimba la Taifa Jumamosi August 10 kuikabili Township Rollers katika mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya awali
Baada ya mafanikio makubwa kupatikana kwenye wiki ya Mwananchi, uongozi wa Yanga umewataka mashabiki wake kutorudi nyuma, sasa wahamishie nguvu zao kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema nguvu ya mashabiki ni silaha muhimu hasa kwa michezo yote itakayopigwa uwanja wa Taifa
"Tunawaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga, kwa ari,upendo na mshikamano ule ule wa juzi na hamasa ya Wiki nzima iendelee kwenye mchezo huo, tujitokeze kwa wingi sana kuipa nguvu timu yetu siku ya mchezo ili kuhakikisha tunapata ushindi"
Mchezo wa Jumamosi una umuhimu wa kipekee kwa Yanga ambayo imerejea kwenye michuano hiyo baada ya kukosa msimu mmoja
Huu ni mchezo wa kisasi, Rollers iliiondosha Yanga ligi ya mabingwa mwaka jana baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa na baadae timu hizo kutoka suluhu kwenye mchezo wa marudiano huko Botswana
cutLakini hakuna ubishi kuwa Yanga ya sasa sio ile. Juzi kwenye mchezo dhidi ya Kariobangi Sharks, imedhihirisha kuwa ni timu tofauti yenye wachezaji ambao wana kiu ya kupata mafanikio
Kwa Yanga hii ya sasa, pamoja na sapoti ya mashabiki wake, haitakuwa rahisi kwa timu yoyote kupata ushindi dhidi yake hasa kwa michezo ya nyumbani
Yanga itaelekea visiwani Zanzibar kesho kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo huo
Ikiwa Zanzibar, Yanga itacheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Mlendege na Malindi
Yanga hii #Imebamba #TambaaNayoKimataifa