Yanga imekuwa ikisuasua kupachika mabao msimu huu ukilinganisha na ilivyofanya misimu mitatu iliyopita ambayo ilifanikiwa kutwaa ubingwa VPL.
Changamoto kubwa iliyoikabili Yanga msimu huu tofauti na misimu mingine ni majeruhi. Wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza hasa Tambwe, Chirwa na Mwashiuya walishindwa kuitumikia Yanga kwenye michezo ya mwanzo wa msimu.
Chirwa na Mwashiuya wamerejea mapema wakati Tambwe amerejea rasmi kikosini mwanzoni mwa wiki hii.
Kurejea kwa Tambwe dimbani kumempa ahueni Lwandamina ambaye sasa washambuliaji wake wote wako fiti.
Lwandamina amesema Tambwe ni mshambuliaji anayejua majukumu yake vizuri na kukosekana kwake kuliipunguzia makali safu yake ya ushambuliaji.
Kurejea kwake ni dhahiri kutaongeza kitu kwenye safu ya ushambuliaji kutokana na aina yake ya uchezaji.

ADVERTISE HERE