Mshambuliaji wa Yanga Juma Balinya amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa jana kwenye kilele cha wiki ya Mwananchi
Balinya alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilicholazimishwa sare ya bao 1-1 na Kariobangi Sharks
Mshambuliaji huyo kutoka Uganda amesema licha ya matokeo hayo, haukuwa mwanzo mbaya kwao
"Tunawashukuru sana Wananchi kwa kuja, hatukuanza vibaya sana," amesema
"Baada ya muda tutakuwa vizuri zaidi kwani tuna kikosi bora. Nawahakikishia mtafurahi kwenye ligi pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa"
Jana mashabiki wa Yanga waliweka rekodi kwa kuujaza uwanja wa Taifa unaochukua mashabiki takribani elfu 60
Licha ya Yanga kutopata ushindi, wachezaji walionyesha uwezo mkubwa
Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa kihistoria Mwinyi Zahera alisema watafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kabla ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers wiki ijayo