Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' iko nchini Kenya ambapo kesho Jumapili itashuka kwenye uwanja wa Kasarani kuumana na Harambee Stars kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za michuano ya CHAN 2020 kwa wachezaji wa ndani
Baada ya kulazimishwa suluhu ya 0-0 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam wiki iliyopita, Stars inahitaji kuibuka na ushindi ugenini ili iweze kusonga mbele
Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo Etienne Ndayiragije amesema wamefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mchezo wa kwanza hivyo wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri ugenini
Amewataka Watanzania kuwaunga mkono kwa maombi na dua ili waweze kushinda mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na upinzani mkali
Timu ya Tanzania iliwasili salama nchini Kenya jana tayari kwa mchezo huo