Kambi Moro yaongeza mzuka Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Aug 2019
Kambi Moro yaongeza mzuka Yanga

Baada ya kujifua kwa wiki mbili mjini Morogoro, Kikosi cha Yanga kimepanga kurejea kesho Ijumaa mchana kisha kujiandaa na mechi yao ya kimataifa dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya itakayopigwa siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi.

Mabosi wa klabu hiyo wamejivunia kambi hiyo ya mjini Morogoro, wakidai imesaidia kwa kiasi kikubwa vijana wao kunoa makali na sasa imefika wakati wa kuwasha moto kwenye michuano ya ndani na ile ya kimataifa wakishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga Hamad Islam amesema kwamba kesho mchana kikosi chao kitaanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam

Islam ambaye alikuwa akiongoza usimamizi wa kambi hiyo sambamba na mjumbe mwenzake Mhandisi Bahati Mwaseba amesema kambi yao imekuwa na mafanikio makubwa

Amesema wakiwa Morogoro wachezaji na makocha wamekuwa katika utulivu mkubwa wa kupata maandalizi ya kutosha katika kujiandaa na msimu mpya

Kiongozi huyo amesema kuwa uongozi wao umeridhika na kazi iliyokuwa inafanyika katika maandalizi hayo ambapo sasa wanarejea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi.

Aidha Islam licha ya kuwapongeza wanachama na mashabiki wa timu hiyo mkoani humo amewataka mashabiki hao kusafiri kwa wingi kwenda kuungana na wenzao katika mchezo wa Jumapili Agosti 4 dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’