Nguvu ya Buku wakarabati wodi Mwananyamala

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jul 2019
Nguvu ya Buku wakarabati wodi Mwananyamala

Yanga Tawi la nguvu ya Buku lenye makazi yake Mwananyamala leo wamekabidhi rasmi msaada wa ukarabati wa Wodi ya Wanaume no.5 waliokuwa wakifanya kwa takribani wiki moja kuelekea kilele cha siku ya Wananchi inatarajiwa kuadhimishwa na Klabu ya Yanga Jumapili ya Agosti 4,2019.

Akizungumza na Wanahabari mara baada ya makabidhiano Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala, Mussa Wambura aliwapongeza Wanayanga tawi la Nguvu ya Buku kwa fikra za msaada walioufikiria na fundisho tosha kwa wengine.

Alisema Wambura, msaada wa kitendo mlichokifanya kitabaki kuwa Historia kwa Hospitali ya Mwanabyamala na kuwaomba jamii ziige kutoa misaada ya namna hii inayomgusa kila binadamu kwani Hospitali ni yetu sote tusiiachie Serikali tu, jukumu hili ni la kila mmoja.Leo mmefanya Tawi la Nguvu ya Buku tunaomba wajitokeze na wengine.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Sindano Mwananyamala ambako Tawi hilo linapatikana aliwapongeza sana Tawi la Nguvu ya Buku kwa kitendo cha Kijamii walichokifanya na hakika yeye kama mpenzi wa upande wa pili wamejifunza kitu ambacho kinastahili kuigwa na Mwananchi yeyote anayejitambua.

Nae Mwenyekiti wa Nguvu ya Buku, Ally Kuacha aliwapongeza wanachama wake kwa kujitoa mpaka kukamilisha mchakato mzima waliokuwa wamekusudia kuelekea kilele cha siku ya Wananchi na kuwaomba waendelee na mshikamano huohuo siku zote.

Mwisho Katibu wa Tawi la Yanga la Nguvu ya Buku, Juma Iyagala alisema ukarabati huo wa Wodi ya Wanaume umegharimu Shilingi 1,830,000/= ambao ni kupaka rangi ndani na nje, kupaka rangi bati pamoja na kubadilisha nyavu za mbu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’