Hatutarudia kosa la kufungwa nyumbani - Mwandila

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jul 2019
Hatutarudia kosa la kufungwa nyumbani - Mwandila

Kufanya kosa sio kosa...kosa ni kurudia kosa ndio msemo ambao mabosi wa Yanga wanautumia kuelekea mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya awali dhidi ya Township Rollers

Yanga itamenyana na Township Rollers kati ya August 09-11 katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa

Mapema mwaka jana, Rollers walicheza na Yanga kwenye raundi ya kwanza ya michuano hiyo na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 2-1

Rollers waliupata ushindi huo jijini Dar es salaam, mchezo wa marudiano ukipigwa Botswana na kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana

Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema kilichoiponza timu hiyo mwaka jana, ni kupoteza mchezo wa nyumbani

Mwandila amesema wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo utakaopigwa jijini Dar es salaam

cut

Licha ya ubora wa kikosi cha Township Rollers, Yanga ina kila sababu ya kushinda mchezo wake wa nyumbani

Usajili makini uliofanywa, kucheza mbele ya mashabiki wake ni sababu kwao kufanya vizuri kwenye mchezo huo

Mwaka jana mashabiki walikata tamaa na timu yao kutokana na mwenendo usioridhisha, lakini hali itakuwa tofauti August 10

Wanayanga kutoka ndani na nje ya jiji la Dar es salaam wanatarajiwa kufurika kwa wingi uwanja wa Taifa kuiunga mkono timu yao

Mabingwa hao wa kihistoria wamejichimbia mkoani Morogoro wakiendelea kujifua kujiandaa na mchezo huo

Augsut 04 watakuwa na mchezo wa kuhitimisha kilele cha wiki ya Mwananchi kwa kuumana na Karioangi Sharks katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’